Huwezi kusikiliza tena

Nkurunziza atoa wiki kukamatwa wauaji

Rais wa Burundi ametoa wiki moja kwa vyombo vya usalama nchini humo kuwakamata watu waliomuua Jenerali Athanase KARARUZA.

Afisa huyo mwandamizi katika jeshi la Burundi aliuawa na mkewe jana katika shambulio la kushtukiza mjini Bujumbura.

Katika hotuba yake kwa taifa jana jioni, Rais NKURUNZIZA ameapa kuangamiza makundi ambayo yamekuwa yanashambulia na kuwauwa maafisa wakuu jeshini na serikalini.

Zaidi sikiliza taarifa ya Ramadhan Kibuga kutoka Bujumbura.