Bodaboda
Huwezi kusikiliza tena

Bodaboda zawafaa wagonjwa Uganda

Pikipiki za abiria maarufu kama bodaboda mbali na kuwasafirisha watu, zinachukiwa na baadhi yao kutokana utovu wa nidhamu wa wale wanaoziendesha.

Lakini jamii ya Katosi- katika wilaya ya Buikwe- Mashariki mwa mji mkuu wa kampala inaona fahari ya bodaboda hizo, kwa sababu ya kuwasaidia kimaisha kwa kuwapeleka katika vituo vya afya kwa kutumiwa kama gari la wagonjwa.

Mwandishi wa BBC Kampala Siraj kalyango ametembelea eneo hilo na kutuandalia taarifa ifuatayo.