Ujangili
Huwezi kusikiliza tena

Majangili watishia ndovu na wahifadhi Kenya

Vita dhidi ya uwindaji haramu vimekuwa vikiimarishwa katika mataifa mengi barani Afrika. Miongoni mwa wahusika katika vita hivyo, ni maafisa wa uhifadhi ambao wamekuwa mstari wa mbele kuyasaidia mataifa kuzuia mauaji ya wanyama pori.

Hata hivyo wawindaji haramu wamekuwa wakiwalenga na kuwauwa. Mapema mwaka huu raia wa Uingereza Roger Gower aliuawa nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Uhifadhi- IRF, matukio ya mauaji ya maafisa hao yamekuwa yakiongezeka kila mwaka na kuathiri juhudi za kuzuia uwindaji haramu.