Getrude
Huwezi kusikiliza tena

Mtoto Mtanzania aliyehutubia mkutano wa UN

Siku chache zilizopita viongozi wa ulimwengu walikutana jijini New York nchini Marekani katika baraza la Umoja wa Mataifa juu ya masuala ya mabadiliko ya tabia ya nchi.

Lakini ni mtoto wa miaka 16 Mtanzania Getrude Clement ndie aliyeteka maskio na macho ya Watanzania wakati alipohutubia baraza hilo kuwawakilisha watoto na vijana wa ulimwenguni kote.

Mwandishi wa BBC Sammy Awami alizungumza na Getrude, na alianza kwa kumuuliza alikuwa anajisikiaje wakati akilihutubia baraza hilo.