Rwanda
Huwezi kusikiliza tena

Vijana watakiwa kutotegemea serikali kwa ajira Rwanda

Serikali ya Rwanda imewahimiza vijana wanaofuzu kutoka vyuo vikuu kufikiria namna wanavyoweza kubuni ajira zao wenyewe badala ya kutegemea kuajiriwa na serikali kama ilivyokuwa desturi.

Hayo yameelezewa wahitimu wa vyuo vikuu nchini Rwanda ambao bado wanatafuta ajira katika siku maalum inayotengwa na serikali kuwakutanisha na wakuu wa makampuni na taasisi mbali mbali ambazo bado zina nafasi ya kazi kwa ajili ya kuwapa fursa kujaribu bahati hayo.

Mwandishi wa BBC Yves Bucyana alihudhuria siku hiyo na kuandaa taarifa hii.