Omar
Huwezi kusikiliza tena

Msanii anayeiga sauti za Magufuli na Kikwete

Fani ya maigizo imekua sana kutokana na mabadiliko ya teknolojia na mfumo wa vyombo vya habari ambapo baadhi ya vijana wenye vipaji hivyo wanatumia fursa hiyo vilivyo.

Kijana Shaffii Omar kutoka nchini Tanzania, ni mmoja wa watu walionufaika na mabadiliko haya na kujizolea umaarufu mkubwa kutokana na uwezo wake wa kuigiza sauti za viongozi, zikiwemo sauti za Rais wa Tanzania John Magufuli na Rais Mstaafu wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.

Mwandishi wa BBC Arnold Kayanda amezungumza na mwigizaji huyo na kwanza akamuuliza alijitosa vipi katika ulingo huo wa kuigiza sauti.