Mtoto
Huwezi kusikiliza tena

Mtoto aokolewa kwenye vifusi vya jengo Nairobi

Mtoto mchanga mwenye umri wa miezi saba, ameokolewa kutoka kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka siku nne zilizopita jijini Nairobi, nchini Kenya.

Jengo hilo lenye ghorofa sitaliliporomoka wakati mvua kubwa ikinyesha siku ya Ijumaa na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 22.

Mtoto huyo ambaye hakupata majeraha yoyote, sasa ameruhusiwa kutoka hospitali na kwenda nyumbani.

Mwandishi wetu Emmanuel Igunza anaripoti zaidi.