Fatacky
Huwezi kusikiliza tena

Wimbo wa Rangi ya Chungwa ulivyopata jina

Zipo nyimbo kadhaa ulimwenguni ambazo kutokana na kurudiwa kuimbwa kutoka kizazi kimoja mpaka kingine, zimeedelea kuwa maarufu mpaka leo.

Wimbo wa Rangi ya Chungwa ukielekea kutimiza miaka hamsini bado unazikonga nyoyo za walio wengi ingawa kwa miaka mingi haikufahamika ni nani hasa aliongoza katika kuuimba.

Apatae Fatacky aliuimba wimbo huu mwanzoni mwa miaka ya sabini akiwa na Nyanyembe Jazz ya kwao Tabora wakati huo akiwa kijana wa miaka 21.

Apatae Fatacky alianza kuimba alipokuwa akisoma katika Shule ya wavulana ya Tabora kabla ya kuchukuliwa na Riko Jazz mjini Bukoba.

Mwandishi wetu Arnold Kayanda amemtembelea Fatacky katika makazi yake yaliyoko Harare, Zimbabwe.