Murage
Huwezi kusikiliza tena

Tatizo la ugonjwa wa shinikizo la damu

Leo dunia inaadhimisha siku ya ugonjwa wa shinikizo la damu, yaani kupanda Presha. Lengo kuu likiwa ni kuwahamasisha wananchi wa mataifa yote jinsi ya kuzuia na kutibu ugonjwa huu, ambao kwa sasa umeenea sana kiasi kuwa janga.

Huku kauli mbiu ya kampeni ya mwaka huu ikiwa ni: 'kila mtu kujuwa iwapo kipimo chake cha presha kipo sawa.

Kwa mujibu wa shirika la afya Duniani (WHO), Afrika inashuhudia ongezeko kubwa zaidi duniani la wagonjwa wa shinikizo la damu, ikiwa ni asilimia 46. Kenya ikiwa mojawapo ya nchi za Afrika.

Mwandishi wa BBC David Wafula alitembelea mmoja wa wanaougua ugonjwa huu, Bw Joram Murage.