SnoCream
Huwezi kusikiliza tena

Biashara ya aiskrimu ya nusu karne Dar es Salaam

Wote tunakumbuka hisia ya furaha tulipokuwa watoto na kupelekwa kununua lambalamba (aiskrimu) - ladha na rangi ya kuvutia pamoja na ubaridi iliposhuka kooni.

Duka la Sno-cream jijini Dar es salaam, limekuwa kitovu cha furaha hiyo kwa watoto na watu wazima, likitengeneza bidhaa hiyo tangu miaka ya uhuru wa nchi hiyo.

Mwandishi wetu Tulanana Bohela ametembelea duka hilo kupata kionjo na kutuletea taarifa ifuatayo.