Kunyonyesha
Huwezi kusikiliza tena

Wanawake wanyonyesha watoto kazini Kenya

Shirika la afya duniani linasema nchi nyingi duniani bado hazijapitisha sheria ambazo zitawasaidia akinamama wenye ajira kuweza kuendelea na kuwanyonyesha watoto licha ya kufanya kazi. Katika ripoti iliyotolewa majuzi iliyochunguza sheria katika nchi 194, takriban humusi yao tu zilikuwa zimezingatia mwongozo wa shirika hilo na kuwa na sheria zinazofaa.

Moja ya nchi hizo ni Kenya. Hivi majuzi Bunge la nchi hiyo limepitisha sheria inayowataka waajiri kutenga chumba cha watoto kutumia wakati wazazi wao wanafanya kazi.

Waajiri wengi wameelezea hofu yao kufuatia kupitishwa kwa sheria hiyo, hata hivyo baadhi ya kampuni kubwa tayari yalikuwa na huduma hizo kazini.

Mwandishi wa masuala ya afya Anne Soy alimtembelea mwajiriwa mmoja wa kampuni ya mawasiliano ya Safaricom na kutuandalia taarifa ifuatayo.