Micheline
Huwezi kusikiliza tena

Raia wa DR Congo mshindi wa tuzo ya Amnesty

Wiki hii shirika la kutetea haki za kibinadamu la Amnesty International imetoa tuzo yake ya haki za binadamu kwa baadhi ya Waafrika walioonesha ukakamavu katika kupigania haki.

Miongoni mwao ni mwanamuziki kutoka Benin Angelique Kidjo ambaye amepokezwa tuzo hiyo pamoja na wanaharakati wengine Y'en a Mare kutoka Senegal, Le Balai Citoyen kutoka Burkina Faso na raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Micheline Mwendike.

Wote hao wametambuliwa kwa kupigana dhidi ya ukiukaji wa haki hasa kutoka kwa vyombo vya utawala katika nchi zao.

Muda mfupi baada ya kutangazwa washindi uBBC imepata fursa ya kuzungumza na Micheline Mwendike wa Congo, ambaye ametueleza harakati zao zinahusu nini hasa.