Olivier
Huwezi kusikiliza tena

Msanii wa Rwanda aliyetunga nyimbo mafichoni

Hivi karibuni tumetembelewa na msanii kutoka Rwanda anayefanya shughuli zake za muziki hapa London.

Ni msanii wa nyimbo za injili. Olivier Nzaramba ametoa albamu yake ya kwanza kwa lugha ya Kinyarwanda, lakini sasa anapanga kutoa albamu mpya kwa lugha ya Kiswahili, Kiingereza na Kinyarwanda.

Anasema mmoja ya nyimbo zake alitunga wakati wa mauaji ya kimbari alipokuwa amejificha yeye na familia yake nchini Rwanda mwaka 1994 bila kujua hata kama watatoka salama.