Wawili wafariki maandamano ya upinzani Kenya

Wawili wafariki maandamano ya upinzani Kenya

Takriban watu wawili wameripotiwa kufariki dunia katika maandamano ya upinzani katika mji wa Kisumu, magharibi mwa Kenya.

Maandamano hayo yanayofanyika sasa kila Jumatatu yalikuwa na ghasia katika mji wa Kisumu magharibi mwa Kenya. Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani alisema waliopigwa risasi na polisi walikuwa waporaji.

Katika mji mkuu, Nairobi, viongozi wa upinzani waliongoza maandamano ya amani wakitaka maafisa wa tume ya uchaguzi wajiuzulu kabla ya uchaguzi mkuu wa mwakani. Chama cha upinzani kimesema maafisa wa tume hiyo wanaelemea upande wa serikali.

Mwandishi wa BBC Anne Soy anatuarifu kutoka Nairobi.