Uhaba wa sukari Tanzania watatiza waislamu

Uhaba wa sukari Tanzania watatiza waislamu

Leo ni siku ya nne ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa wailamu kote duniani.

Hata hivyo wakati waislamu wakiendelea na mfungo, nchini Tanzania tatizo la kukosekana kwa sukari huenda likaathiri mfungo huo kufuatia kuongezeka kwa matumizi ya bidhaa hiyo.

Sukari hutumika kwenye vyakula vinavyotumika wakati wa' kufuturu' yaani kuvunja mfungo kama vile tambi, chai, uji, maji ya matunda na vingine vingi.

Serikali ya Tanzania mbali na kuahidi kuagiza sukari kutoka nje ili kuziba pengo la upungufu uliopo kwa sasa, lakini bado upatikanaji wake umeendelea kuwa nadra.

Mwandishi wetu wa Dar es Salaam David Nkya ameandaa taarifa ifuatayo.