Redio na TV zafunga matangazo DRC

Redio na TV zafunga matangazo DRC

Baadhi ya vituo vya redio na runinga katika mji mkuu Kinshasa, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zimefunga matangazo yake kuanzia leo, ikiwa ni ishara ya kuanza mgomo kufutia makampuni ya simu za mikononi kupandisha gharama za huduma za intaneti.

Ni karibu majuma matatu sasa, tangu gharama ya huduma hiyo muhimu ilipoongezwa ghafla kwa asilimia mia moja.

Na ili kushinikiza serikali na makampuni hayo kupunguza gharama za intaneti, raisi wa muungano wa wandishi wa habari nchini humo alitoa mwito kwa viongozi wa vyombo vya habari kufunga matangazo hii leo Jumatatu.

Tumezungumza na mwandishi wetu wa Kinshasa Mbelechi Msoshi na akatueleza kinachojiri huko.