Referendum
Huwezi kusikiliza tena

Waafrika Uingereza na kura ya maoni ya EU

Uingereza inafanya kura ya maoni wiki hii kuamua iwapo isalie katika Muungano wa Ulaya au ijiondoe.

Kwa mujibu wa sensa iliyofanywa mwaka 2011, kuna zaidi ya Waafrika milioni moja nchini Uingereza, wakiwemo wale waliozaliwa hapa na wale waliohamia hivi karibuni.

Hawa wote sauti yao ni muhimu sana katika kura hii. Lakini ni kwa kiasi gani wamejihusisha na kampeni au hata kujishughulisha katika kura hii ya maoni?

Dayo Yusuf amekwenda kuzuru mji wa Bristol, ulio maarufu sana kwa jamii ya Waafrika hasa Wasomali na ametuandalia taarifa hii.