Bemba
Huwezi kusikiliza tena

Mbabe wa vita DRC Bemba afungwa miaka 18

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita (ICC) mjini The Hague imemhukumu makamu wa rais wa zamani nchini DR Congo Jean-Pierre Bemba kifungo cha miaka kumi na minane gerezani kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na makosa ya kivita.

Bwana Bemba alikutwa na hatia ya kushindwa kuzuia vikosi vyake kufanya mauaji na ubakaji kwa raia katika Jamhuri ya Afrika ya Kati baina ya mwaka 2002 na 2003.

Mawakili wake wamesema watakata rufaa.

Zawadi Machibya anaarifu zaidi.