Wakimbizi Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Maisha ya wakimbizi kambini Tanzania

Wakati dunia inaadhimisha siku ya wakimbizi Duniani idadi ya wakimbizi na wengine wanaokimbia makazi yao imevunja rekodi duniani.

Mpaka mwishoni mwa mwaka jana ilifikia watu milioni sitini na tano na laki tatu, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Umoja huo unasema mateso na vita katika nchi kama Syria na Afghanstan vimelazimisha kuongezeka kwa idadi ya watu wanaokimbia makazi yao.

UNHCR linasema wastani wa watu 24 wanakimbia makazi kila dakika, kila siku, na nusu yao ni watoto.

Huku wasichana wengi wakiwa katika hofu ya kunyanyaswa kijinsia na ubakaji.

Sammy Awami ana taarifa zaidi