Sudan kusini na uchunguzi wa UN

Sudan kusini na uchunguzi wa UN

Umoja wa Mataifa unasema matokeo ya awali ya uchunguzi dhidi ya mashambulizi mabaya kuwahi kutokea Sudan Kusini inaonesha mkanganyiko juu ya amri na mamlaka vilivyoathiri mwitikio .

Shirika la misaada ya kibinaadamu MSF limesema kwamba walinda amani walichukua zaidi ya saa sita kuchukua hatua,na katika kipindi hicho watu thelathini wanaarifiwa kupoteza maisha na wengine zaidi ya mia moja kujeruhiwa wakati wa shambulio lililotokea mwezi wa February.

Raia zaidi ya elfu hamsini walitafuta hifadhi katika makambi, katika uchunguzi uliofanywa tofauti tofauti, Umoja wa mataifa unavishutumu vikosi vya serikali ya Sudani Kusini kwa mashambulizi dhidi ya raia.

Kutokana na uchunguzi huo wa umoja wa mataifa, Regina Mziwanda alizungumza na mchambuzi wa masuala ya Sudan Kusini na Afrika kw aujumla Mohammed Jaffer na kumtaka aeleze zaidi kuhusu ripoti hiyo