Kura ya maoni Uingereza ni leo

Kura ya maoni Uingereza ni leo

Leo raia wa Uingereza wanapiga kura ya maoni asubuhi hii kuamua iwapo Uingereza isalie au ijiondoe katika Muungano wa Umoja wa Ulaya.Wapiga kura watajibu swali moja kwamba Uingereza ibakie kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya au ijiondoe katika Umoja wa Ulaya.

Zaidi ya Waingereza milioni arobaini na sita wanatarajiwa kupiga kura hiyo ya maoni.Kwa mara ya mwisho Uingereza kuendesha kura maoni kuhusu uanachama wake ndani ya Umoja huo uliojulikana kwa wakati huo Jumuiya ya Uchumi ya Ulya ilikuwa ni miaka aroboini iliyopita.

Hata hivyo kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa BBC haitaweza kukuletea matangazo ya uchaguzi huo moja kwa moja hadi hapo vituo vitakapofungwa na kura kuhesabiwa, hata hivyo kwa ufafanuzi zaidi Regina Mziwanda alizungumza na Zawadi Machibya aliyeko London na kwanza nilitaka kujua vituo vitafunguliwa saa ngapi.