Wakimbizi wa Eritrea waandamana Ethiopia

Wakimbizi wa Eritrea waandamana Ethiopia

Mamia ya wakimbizi kutoka Eritrea waishio Ethiopia wameandamana katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa wakiunga mkono taarifa ya hivi majuzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu Eritrea.

Madai ya Umoja wa Mataifa ni pamoja na mauaji, utumwa wa ngono na watu kulazimishwa kufanya kazi, lakini serikali ya Eritrea imesema ripoti hiyo ina malengo ya kisiasa na haina msingi wowote.

Emmanuel Igunza ametutumia taarifa hii kutoka Addis Ababa.