eco_manyatta
Huwezi kusikiliza tena

Mradi unaoimarisha nyumba za Wamasai Kenya

Kwenda na wakati ndio msemo unaotumika sana nyakati hizi za technolojia na utandawazi. Mfano fika unaonekana katika jamii ya kimaasai nchini Kenya, inayojulikana kwa kukumbatia utamaduni wake,sasa imekubali kuwa nyumba zao za kijadi yani manyatta zinafaa kuimarishwa kwani zimepitwa na wakati. Mradi wa Eco Manyatta umetoa fursa ya kujenga nyumba hizo kwa kutia nakshi za kisasa. Ng'endo Angela ametembelea County ya Laikipia ngome ya Wamaasai nchini Kenya kujionea mradi huu unawanufaisha vipi.