Wailsmau wa Uingereza
Huwezi kusikiliza tena

Waislamu wafunga mda mrefu zaidi Uingereza

Waislamu nchini Uingereza wanafunga muda mrefu zaidi mwaka huu katika kipindi cha miaka thelathini na mitatu iliyopita, kutokana na mwezi wa Ramadhani kwenda sambamba na majira ya joto. Ikimaanisha kuwa wanafunga saa nyingi zaidi kwa siku. Watoto hasa wale wanaofanya mitihani shuleni huenda wakaona ni changamoto kubwa kuhimili muda huo mrefu. Na walimu pia wamezungumzia kuhusu hili. Zuhura Yunus alitembelea shule ya Riverside mjini London na kutuandalia taarifa ifuatayo.