Kagame na Magufuli waahidi kuimarisha uhusiano

Kagame na Magufuli waahidi kuimarisha uhusiano

Rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenzake wa Tanzania John Magufuli wameahidi kudumisha ushirikiano wa mataifa hayo mawili ili kuwawezesha raia wao kufanya kazi pamoja kwa manufaa ya maendeleo.

Rais Kagame yuko Tanzania kwa ziara rasmi,ambayo wadadisi wa mambo wanasema ni juhudi za kidiplomasia katika harakati za kumaliza uhasama wa miaka kadhaa baina ya mataifa hayo mawili ya Afrika mashariki.

Chini ya Utawala wa Jakaya Kikwete uhusiano baina ya Tanzania na Rwanda ulidorora sana kufuatia mzozo wa kidiplomasia na tofauti za kisiasa.

Kutoka Dar es Salam hii hapa taarifa yake John Solombi.