Waandamana kupinga mauaji ya polisi Kenya

Waandamana kupinga mauaji ya polisi Kenya

Mamia ya watu, wakiwemo mawakili, wameandamana jijini Nairobi, Kenya kupinga mauaji ya kiholela ambayo yanadaiwa kutekelezwa na polisi nchini humo.

Maandamano hayo yamefanyika kufuatia kupatikana kwa miili ya wakili Willie Kimani, mteja wake Josephat Mwendwa na dereva wa teksi Joseph Muiruri.