Netanyahu ziarani Ethiopia

Netanyahu ziarani Ethiopia

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu yupo mjini Addis Ababa akikamilisha ziara yake barani Afrika baada ya kutembelea nchi nne barani humo. Miongoni mwa shughuli zake wakati wa ziara yake ya siku moja nchini Ethiopia, Bwana Netanyahu alilihutubia bunge. Mapema leo aliahidi kundi la kwanza la Wayahudi Waethiopia 9000 watasafirishwa kwenda Israel baada ya kusubiri miaka chungu nzima ya kutaka kuungana na familia zao. Emmanuel Igunza anaarifu zaidi.