Raia wa Nigeria ashinda tuzo ya Komla Dumor

Raia wa Nigeria ashinda tuzo ya Komla Dumor

Kwa miaka mingi, jina Komla Dumor, limekuwa likihusishwa na ubora wa hali ya juu katika masuala ya utangazaji hapa BBC.

Komla ambaye alikuwa mstari wa mbele kwa namna mbalimbali alichochewa na hali ya uhitaji wa kueleza habari za Afrika ambazo, hutoa taswira halisi.

Shirika la habari la BBC lilizindua tuzo kwa heshima ya aliyekuwa mtangazaji wake Komla Dumor, mwaka wa 2014 baada ya kifo chake akiwa na umri wa miaka 41.

Tuzo hiyo hutambua umahiri na vipaji vya watangazaji wa Kiafrika.

Hii leo ametangazwa mshindi wa pili wa tuzo ya Komla Dumor, anaitwa Didi Akinyelure kutoka Nigeria.