Fahamu iwapo unaweza kuwa Mwanaolimpiki
Je, una mtazamo wa Mwanaolimpiki?
Jaribu kujibu maswali haya ya sekunde 60 na uone unahitaji nini kushinda dhahabu, licha ya uwezo wako kimichezo.
Una umri gani?

Je, wewe ni mtu wa kufanya mambo haraka haraka au kwa umakinifu?
Maoni ya mtaalamu
Ikiwa wewe hufanya kazi kwa ufasaha na umakinifu unaweza kufanikiwa katika mambo mengi maishani, ikiwemo michezo. Ikiwa sivyo, ni wakati wa kubadilika.

hufanya juhudi 110% au hufanya mambo kiurahisi?
Maoni ya mtaalamu
Kujiwekea malengo ya juu sana kunaweza kumsaidia mwanariadha bingwa, lakini pia ni muhimu kutokuwa mkali sana kwa mwili wako na kuhakikisha malengo yako ni ya uhalisia.

Hupaa au hukwama mambo yanapokuwa magumu?
Maoni ya mtaalamu
Uko kwenye mstari wa kuanza mbio za mita 100 na mamilioni ya watu wanakutazama - unaweza kumudu presha? Mabingwa hufana presha ikiwa juu.

Je, wewe ni nyota mpenda sifa au mtu wa kujionea haya?
Maoni ya mtaalamu
Ingawa labda si moja ya sifa zinazopendwa sana, wale wenye kujisifu wanaweza kufanikiwa kama wanariadha. Lakini si wanariadha wote bingwa wana sifa hizi, kumbuka, hakuna anayependa wanaojisifu!

Hukabili wapinzani au hutafuta mashindano rahisi?
Maoni ya mtaalamu
Huwezi ukawa bingwa wa Olimpiki iwapo unataka kushindana na watu utakaowashinda. Huwa na moyo wa ushindani kutasaidia kukuimarisha zaidi.

Huwa unaanza sherehe au wasubiri mwaliko?
Maoni ya mtaalamu
Mambo mema huwa hayawafikii wanaoketi kitako. Ukihukua hatua na kudhibiti mambo ndipo utakapofanikiwa.

Huwa wafanya mambo kwa kupenda au kwa kutafuta manufaa?
Maoni ya mtaalamu
Una msukumo kiasi gani? Hili sana hupatikana katika matangazo ya nafasi za kazi, kwa sababu - kuwa na msukumo ni moja ya kiungo muhimu katika kufanikiwa.

Wapenda maeneo salama au hatari?
Maoni ya mtaalamu
Mpinzani wako mkali zaidi yumo kwenye kioo. Iwapo umeangazia sana kujiimarisha, viwango vyako, kuna uwezekano kwamba utaenda mbali.

Hujiamini na kufaa au hujifuta kazi?
Maoni ya mtaalamu
Kujiamini ni muhimu sana katika kufanikiwa michezoni - mwulize Usain Bolt ... Lakini hili linaweza kubadilika, ukitegemea hali kwa hivyo hata Usain wakati mwingine atajishuku.

Huwa na mwelekeo au husahau sana?
Maoni ya mtaalamu
Kwa hivyo bado tuko pamoja? Umefanikiwa kufika hapa bila kupoteza mwelekeo? Ubongo unaweza tu kuangazia vitu vichache sana kwa wakati mmoja kwa hivyo kuangazia mambo muhimu ni muhimu sana.

Ufanye mambo kivyako au uombe usaidizi?
Maoni ya mtaalamu
Binadamu si kisiwa. Unahitaji usaidizi? Waombe wenzako, jamaa, marafiki, kocha - wanaweza kusaidia kuimarisha uwezo wako.

Kuongozwa na malengo au kutumai mema?
Maoni ya mtaalamu
Unapotimiza malengo yako, huwa unajiamini zaidi katika uwezo wako na kabla ya ufahamu yanayojiri, utakuwa umetimiza mambo makubwa.

Huwa unafanya mazoezi?
Mtazamo wako ni:





Sifa zako kuu ni , , na .
Lakini unaweza kujiimarisha katika , , na .

Njia
Maswali haya yaliandaliwa kwa ushirikiano na Dkt David Fletcher, mtaalamu wa saikolojia ya michezo kutoka Chuo Kikuu cha Loughborough. Maswali haya yalitayarishwa kuonyesha sifa za muhimu za kiakili ambazo ni muhimu katika kuwa na ushindani michezoni.
Waliochangia
Imeandaliwa na Ashleigh Jackson, Scott Jarvis, Nathan Mercer na John Walton.