Kamati ya Olimpiki yaweka sheria kali ,Rio

Bendera ya michuano ya Olimpiki na ya urusi zikipepea Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Urusi yathibitishwa kushiriki michuano ya Olimpiki

Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki,Thomas Bach,ametangaza kwamba udanganyifu wa utumizi wa dawa za kulevya katika michuano ya Rio tabia hiyo itakuwa haina mahali pa kujificha.

Akizungumza katika usiku wa kuelekea katika sherehe za ufunguzi,Mr Bach amesema kwamba wakati wa michuano hiyo maelfu ya vipimo vitafanywa ,na sampuli za vipimo hivyo zitahifadhiwa kwa miaka kumi ijayo , na kusema kwamba atahakikisha watumizi wote wa dawa za kusisimua misuli kamwe hawatakuwa salama.

Bach Aliongeza kusema kuwa takwimu ya mwisho juu ya idadi ya wanariadha wa Urusi ambao wataruhusiwa kushiriki katika michuano hiyo ya michezo ya Olimpiki watatangazwa saa chache zijazo.

Wakala wa kuzuiautumizi wa dawa za kusisimua misuli imependekeza kuwa yeyote atakayekutwa ametumia dawa hizo wapigwe marufuku katika michuano hiyo chini ya mpango wa ufadhili wa serikali ,ingawa Kamati ya Olimpiki ya Urusi imesema kwamba wanamichezo wake wapatao mia mbili na sabini na mmoja wamesha thibitishwa kushiriki katika michuano hiyo ya Olimpiki