ANC yatarajia matokeo mabaya ya uchaguzi

Makao ya kuhesabia kura Afrika Kusini Haki miliki ya picha AFP
Image caption Makao ya kuhesabia kura Afrika Kusini

Huku matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa kimaeneo yakitarajiwa kutolewa leo, imebainika wazi kuwa chama cha ANC kimeibuka na matokeo mabaya zaidi ya uchaguzi kuwahi kushuhudiwa.

Chama cha Democratic Alliance kimeibuka na ushindi mkubwa na muhimu katika baraza la manispaa ya Nelson Mandela Bay.

Chama cha ANC kinajitahidi kuchukua udhibiti wa miji ya pretoria na Johannesburg.

Hata hivyo, ANC inasalia kuwa chama maarufu katika siasa za Afrika Kusini, kwa kuzoa aslimia 54 ya kura hizo.

Chama cha Democratic Alliance, kimekuwa kikiungwa mkono na wazungu pamoja na chotara, japo wapiga kura weusi wameanza kukiunga mkono, kwa kukatishwa tamaa na mwendo wa kobe wa uimarishaji wa uchumi wa chama tawala cha ANC, na sakata nyingi zinazomkabili rais Jacob Zuma.

Mada zinazohusiana