Mambo muhimu kuhusu Michezo ya Olimpiki

Olimpiki Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mataifa 205 yanashiriki michezo hiyo

Michuano hii ina historia ndefu sana.Ilianza miaka ya 776 kabla ya kuzaliwa kwa Kristo.

Waanzilishi wake walijizatiti kwa miungu wa Kiolimpiki na walivuka kipindi cha kale katika maeneo ya Olimpia. Waliendelea kwa karibu karne 12, mpaka pale Mfalme Theodosius alipotoa amri mwaka 393 baada ya kuzaliwa kwa Kristo kuwa wasiokua na dini wapigwe marufuku .

Katika michuano ya mwaka huu, jumla ya wachezaji 10,500 wanatarajiwa kushiriki haya yakiwa ni mashindano ya 28 ya Olympiki, ya kisasa, na wakati huu yakifanyika mjini Rio Nchini Brazil.

Mataifa 205 yanashiriki michuano hiyo, ambapo kwa mara ya kwanza timu za wakimbizi kutoka Kosovo na Sudan Kusini zitashiriki na kufanya michuano hiyo kufana Zaidi.

Michezo 42 itachezwa huku medali 306 zikishindaniwa katika michuano hiyo, Ufunguzi wa mashindano hayo unafanyika katika dimba la Maracana huku viwanja 33 vikitarajiwa kutumika mjini Rio, na 5 katika majiji ya ya Sao Paulo, Belo Horizonte, Salvador, Brasilia na Manaus

Kabla ya ufunguzi washiriki hao walipata fursa kutizama baadhi ya vivutio vinavyopatikana katika Jiji la Rio ikiwemo ufukwe wa glamorous, Copacabana na Ipanema.

Hali ya ulinzi na usalama Nchini Brazil imeimarishwa ambapo zaidi ya walinzi 85,000 kutoka mataifa 55 wameandaliwa ili kuimalisha ulinzi viwanjani, viwanja vya ndege, barabarani na kwenye maeneo yote ambapo michuano hiyo itafanyika.

Huku mashindano hayo yakifunguliwa Ijumaa nchini humo bado hali ya kisiasa si shwari

Haki miliki ya picha PA
Image caption Maafisa 85,000 watatumiwa kudumisha ulinzi wakati wa mashindano hayo

Washiriki wa Urusi walikuwa na wakati mgumu huku wakihusishwa na kashfa ya matumizi ya madawa ya kusisimua misuli, sababu iliyochangia kamati ya Olympic kujadili hatma ya washiriki kutoka nchini humo.

Miongoni mwa nyota wanaotarajia kung'ara ni muogeleaji mwenye medali 22 kutoka Marekani Michael Phelps, mkimbiaji Usain Bolt na mwanasoka Neymar da Silva Santos JĂșnior maarufu kama Neymar.

Zaidi ya tiketi milioni moja kati ya milioni saba na laki tano bado hazijanunuliwa, huku zaidi ya watalii laki tano wakitarajawa kuingia nchini humo ndani ya kipindi cha michuano hiyo.

Nchi zitakazoshiriki kwa upande wa Afrika Mashariki ni Kenya, Uganda, Burundi, Tanzania na Rwanda.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii