Mwanandondi wa Morocco akamatwa kwa unyanyasaji Rio

Hassan Saada Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hassan Saada alikuwa amepangiwa kupigana kesho

Polisi mjini Rio de Janeiro wanasema wamemkamata mwanamichezo raia wa Morocco kwa tuhuma za unyanyasaji wa kimapenzi.

Mwanabondia, Hassan Saada, anatuhumiwa kuwanyanyasa wafanyakazi wawili wa kike wa kufanya usafi katika Olympic Village, eneo wanamoishi wanamichezo, siku ya Jumatano.

Jaji ameagiza mwanamichezo huyo azuiliwe kwa siku 15 huku polisi wakifanya uchunguzi wao.

Saada alipangiwa kupigana pambano lake la kwanza dhidi ya Mehmet Nadir wa Uturuki hapo kesho.