Paul Pogba: Nyota anayesakwa na Manchester United aitwa Juventus

Paul Pogba Haki miliki ya picha AFP
Image caption Paul Pogba aliondoka Manchester United na kuhamia Juventus mwaka 2012

Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri amesema amemtaka mchezaji anayetafutwa sana na klabu ya Manchester United Paul Pogba afike mazoezini siku ya Jumatatu.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekuwa likizoni Marekani baada ya kumalizika kwa michuano ya Euro 2016.

Pogba, 23, amekuwa akihusishwa na kuhamia Old Trafford kwa bei ya kuvunja rekodi ya dunia ya ununuzi wa wachezaji ya pauni milioni moja.

Meneja wa United Jose Mourinho alikuwa amedokeza kwamba klabu hiyo ilikuwa imekaribia sana kumpata Pogba.

"Kwa sasa, Pogba ni mchezaji wa Juventus," amesema Allegri.

United wataanza msimu kwa mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Leicester City Jumapili.

Juventus wataanza msimu wao Serie A wiki moja baadaye tarehe 20 Agosti.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii