Mitindo iliyovuma ufunguzi Olimpiki Rio 2016
Huu hapa ni kusanyiko wa picha za mitindo na tamaduni zilizovutia watu sana katika mitandao ya kijamii wakati wa sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Rio, 2016.

Chanzo cha picha, ESTEBAN BIBA/EPA
Mavazi ya kitamaduni … na viatu kutoka Burundi
Chanzo cha picha, OLIVIER MORIN/AFP
Shelly-Ann Fraser-Pryce kutoka Jamaica aling'aa kwa mtindo wake wa nywele
Chanzo cha picha, Reuters
Wanamichezo kutoka India nao walivutia kwa koti zao na sari
Chanzo cha picha, LEON NEAL/AFP
Ureno mtindo wao ulikuwa wa jeans
Chanzo cha picha, FRANCK FIFE/AFP
Indonesia waliamua kuvalia kifalme
Chanzo cha picha, Cameron Spencer/Getty
Bermunda nao wakavumisha kaptula za Kibermunda
Chanzo cha picha, LEON NEAL/AFP
Mbeba bendera huyu wa Tonga alisisimua wengi kwa kifua chake wazi kilichong'aa kutokana na mafuta
Chanzo cha picha, Reuters
Norway walitikisa ukumbi kwa vazi hili
Chanzo cha picha, Reuters
Kwa Msumbiji, mashati yenye michoro ya vijisanduku ndiyo yalikuwa mavazi ya sherehe
Chanzo cha picha, Reuters
Kina dada wa Brazil walijitokeza na vazi lenye muundo wa majani, wakiwakilisha rangi ya bendera la taifa lao. Brazil ndio wenyeji.