Meneja wa Kenya aliyeitisha hongo afurushwa Rio

Mkurugenzi wa shirika la kupambana na madawa ya kuongeza nguvu mwilini ADAK Japhter Rugut ameahidi kuchunguza madai hayo kikamilifu. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kenya yakabiliwa na madai mapya ya utumizi wa madawa

Meneja wa timu ya taifa ya Kenya ya riadha katika michezo ya Olimipiki Meja mstaafu Michael Rotich, atahojiwa na kitengo cha jinai pindi atakapowasili Nairobi.

Waziri wa michezo wa Kenya Dr. Hassan Wario, aliyeko mjini Rio de Janeiro amethibitisha kuwa meneja huyo wa timu ya riadha ameamrishwa kurejea nyumbani mara moja.

''kwa hakika hatutavumilia mtu yeyote ambaye anaonesha dalili za kuyumbisha kampeini yetu dhidi ya madawa ya kusisimua misuli''

Gazeti la Sunday Times la jijini London, limetoa ukanda mpya wa video unayoonyesha Meja Michael Rotich, akiahidi kuwaonya wanariadha wa kikosi chake kuhusu ziara ya maafisa wa mamlaka kuu ya kudhidbiti matumizi ya dawa ilizopigwa marufuku , madamu tu alipwe mlungula wa pauni elfu kumi £10,000.

Meja Rotich ni meneja mkuu wa kikosi cha wanariadha wa Kenya.

Ilani ya mapema anasema ,itawapa wanariadha muda wa kusafisha chembechembe za dawa hizo kutoka mwilini mwao.

Meja Rotich anaripotiwa kukanusha kuwa hajafanya lolote baya, huku akiongeza kuwa alizungumza na maripota hao wa kujificha, ili kutaka kuwafahamu ni akina nani hasa na nini walichokuwa wakikitafuta.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ritaa Jeptoo mmoja kati ya zaidi ya wanariadha 40 wa Kenya waliopigwa marufuku

Gazeti hilo la Sunday Times na runinga ya Ujerumani ARD zilimrekodi afisa huyo bila yeye kujua kuwa alikuwa akirekodiwa.

Mkurugenzi wa shirika la kupambana na madawa ya kuongeza nguvu mwilini ADAK Japhter Rugut ameahidi kuchunguza madai hayo kikamilifu.

Madai hayo yanatokea siku mbili tu baada ya shirika la kupambana na madawa duniani WADA kuiondoa Kenya kwenye orodha ya mataifa ambayo yanakiuka kanuni za vita dhidi ya udanganyifu michezoni na utumizi wa madawa ya kusisimua misuli.

Kwa mujibu wa mwandishi mpekuzi Hajo Seppelt, Meja Rotich amekuwa akishirikiana na watu wanaoendesha mpango huo wa siri wa kutoa dawa za kusisimua misuli.

Meja huyo alikuwa miongoni mwa kikosi cha kenya kilichoshiriki katika guaride la ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ijumaa iliyopita.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii