Zlatan Ibrahimovic aliifungia Manchester United bao la ushindi dhidi ya Leicester City na ngao ya Community.
Vijana wa Jose Mourinho walisajili ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mabingwa watetezi wa kombe la EPL msimu uliopita Leicester .
Mechi hiyo ilikuwa ya kuashiria kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya Uingereza EPL.