Mwanaolimpiki anayefanana nawe Rio

Samahani, kisakuzi chako hakiwezi kufungua. Fuatalia habari za BBC kuhusu Rio 2016 hapa

Utaratibu upi umefuatwa kukuchagulia wanamichezo hawa?

Wanamichezo zaidi ya 10,000 kutoka kwa wanamichezo 11,500 watakaoshiriki, ambao maelezo yao yamo kwenye takwimu za Shirikisho la Data la Olimpiki (ODF) wamejumuishwa kwenye mradi huu. Wanamichezo ambao hawakujumuishwa ni kwa sababu maelezo kuhusu kimo chao, uzani na umri hayakupatikana. Takwimu hizi ni kutoka kwa ODF na ni sahihi kufikia Jumatatu 8 Agosti 2016.

Kulinganishwa kwa data yako na hazinadata ya wanamichezo kulifanywa kwa kutumia mfumo wa kufanya hesabu ufahamikao kama Euclidean Distance.

Hesabu hii huwezesha maelezo kuhusu mhusika na wanamichezo wote kuhesabiwa. Wanamichezo ambao wako karibu sana na mhusika kisha hulinganishwa na kimo na uzani wa mhusika.
Iwapo wanamichezo zaidi ya watatu wanakaribia kwa njia sawa mhusika, basi tarehe ya kuzaliwa kwa mhusika hutumiwa kuwatenganisha.


Waliochangia

Imeandaliwa na Nassos Stylianou, John Walton na Nathan Mercer. Utathmini wa data ulifanywa na Ransome Mpini, usanifu ukafanywa na Gerry Fletcher na utekelezaji ukafanywa na Luke Ewer na Chris Ashton. Kazi ya ziada ilifanywa na Liam Bolton na Phil Dawkes