Hakimu nchini Brazil kuruhusu maandamano ya amani

Baadhi ya mashabiki wakionekana wamebeba mabango yenye ujumbe unaosema "Temer nje" katika mashindano ya Olympiki
Image caption Baadhi ya mashabiki wakionekana na mabango yenye ujumbe unaosema "Temer nje" katika mashindano ya Olympiki

Hakimu huko nchini Brazil ameruhusu maandamano ya amani ya kisiasa wakati wa michezo ya olimpiki inayoendelea huko mjini Rio.

Maamuzi hayo yamekuja baada ya waandamanaji hao kufukuzwa katika viwanja mbalimbali vya Olympiki kwa kubeba mabango ya kumkosoa Rais wa mpito, Michael Temer.

Uhuru wa kujieleza

Hakimu amesema kuwa kuwaondoa waandamanaji hao ni ukiukwaji wa uhuru wa kujieleza. Amepokea maombi ya kuruhusu maandamano hayo kutoka kwa chombo cha serikali cha kutetea maslahi ya umma, hata hivyo, waandaji wa michezo hiyo wanatarajia kupinga uamuzi huo.