Afrika yashinda nishani yake ya 5 Rio

Michezo ya Olimpiki inaingia siku yake ya sita leo hii mjini Rio de Janeiro huku Misri na Tunisia ikiongeza idadi ya medali za bara la Afrika kuwa tano kwa jumla

Sara Ahmed wa Misri Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sara Ahmed wa Misri amepata fedha mchezo wa kunyanyua uzani

Medali hizo tatu za Afrika zimepatikana kupitia timu za Misri na Tunisia.

Sara Ahmed na Mohammed Ihab wote wa Misri wamepata fedha mchezo wa kunyanyua uzani naye Ines Boubakry wa Tunisia akajituliza na shaba mchezo wa fencing...

Afrika sasa ina jumla ya medali tano baada ya Afrika Kusini kushinda fedha mbili katika mchezo wa kuogelea.

Afrika Kusini ni ya 31 ikiwa pamoja na Indonesia na New Zeland.

Misri ni ya 43 ikiwa pamoja na Uzbekistan huku Tunisia ikishikilia nafasi ya 45 pamoja na mataifa mengine sita yakiwemo Ureno na Israel..

China ingali inapumua mgongoni mwa Marekani ikiwa katika nafasi ya pili na jumla ya dhahabu kumi, na Marekani inaongoza na dhahabu 11.

Kwa jumla Marekani ina medali 32 na 23.

Japan ni ya tatu ikifuatiwa na Australia, Hungary na Urusi ya sita.

Katika baadhi ya michezo iliyofanyika jana Columbia ilishinda Nigeria kwa mabao 2-0.

Nigeria iliibuka mshindi kundi B na sasa itakutana na Uingereza mechi ya robo-fainali.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kenya imeshindwa mechi zote nne ilizocheza Rio

Afrika Kusini ilienda sare bao 1-1 na Iraq kundi A lakini imeyaanga mashindano kwa kumaliza ya mwisho kundi A..

Senegal ilichapwa na Canada vikapu 68-58 katika mechi ya mpira wa kikapu.

Senegal sasa imepoteza mechi zake zote tatu.

Katika mchezo wa raga Afrika Kusini ilifuzu kwa nusu-fainali ilipoilaza Canada 22-5 na itakutana na Uingereza.

Ndondi

Ilikua ni siku mbaya kwa mabondia wa Kenya kwani wote wawili waliocheza jana, Peter Mungai na Benson Gicharu walipoteza mapigano yao, na leo hii bondia mwingine wa Kenya Rayton Okwiri anazipiga na bingwa wa dunia Mohammed Rabii wa Morocco.

Hatimaye mashindano ya riadha yanaanza kesho kukiwa na fainali ya mbio za mita elfu kumi za wanawake, na za wanaume zitafanyika Jumamosi...