Leicester City wachapwa 2-1 na Hull mechi ya kufungua msimu

Wachezaji wa Hull Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Snodgrass amefunga bao la ushindi dakika ya 55

Mabingwa watetezi wa Ligi ya England Leicester City wameanza msimu wa 2016/17 kwa kuchapwa ugenini na Hull City.

Leicester wamechapwa 2-1, mabao ya Hull yakifungwa na Adama Diomande (46+2') na Robert Snodgrass (55').

Bao la kufutia machozi ya Leicester City limefungwa na Riyad Mahrez kupitia mkwaju wa penalti dakika ya 47.

Haki miliki ya picha PA

Leicester City ndio mabingwa wa kwanza watetezi kushindwa mechi ya kwanza ya msimu uliofuata kutwaa ubingwa enzi ya Ligi ya Premia.

Matokeo ya mechi zilizochezwa Jumamosi

  • Hull 2-1 Leicester
  • Burnley 0-1 Swansea
  • Crystal Palace 0-1 West Brom
  • Everton 1-1 Tottenham
  • Middlesbrough 1-1 Stoke
  • Southampton 1-1 Watford