Olimpiki Rio 2016: Kariman Abuljadayel aweka historia kwa Saudia 100m

Kariman Abuljadayel (kushoto) Haki miliki ya picha AFP
Image caption Abuljadayel alimaliza wa saba kati ya wanariadha wanane waliochuana kundi 3 hatua ya kufuzu ya awali

Mkimbiaji wa mbio fupi Kariman Abuljadayel amekuwa mwanamke wa kwanza kutoka Saudi Arabia kushiriki katika mbio za 100m Olimpiki.

Abuljadayel, 22, aliyekuwa amevalia vazi la kujifunika mwili pamoja na hijab, hakufanikiwa kufuzu baada ya kumaliza nambari saba kundi la tatu la wanariadha wanane walioshindana hatua ya awali ya kufuzu.

Haki miliki ya picha AFP

Muda wake ulikuwa sekunde 14.61.

Raia wa Afghanistan Kamia Yousufi pia alikimbia akiwa amevalia hijab na vazi la kujifunika vyema mwili, na ndiye aliyemaliza wa mwisho kundi hilo muda wake ukiwa sekunde 14.02.

Mwanariadha wa mbio za wastani Sarah Attar alikuwa mwanamke wa kwanza kuwakilisha Saudi Arabia kwenye mashindano ya mbio Olimpiki, aliposhiriki Michezo ya London 2012.

Saudi Arabia ilikuwa imewapiga marufuku wanawake kushiriki Olimpiki lakini marufuku hiyo ikaondolewa 2012.

Mada zinazohusiana