Chama kikuu cha upinzani kinataka kura zihesabiwe tena Lusaka, Zambia

Raia wa Zambia kwenye foleni wakisubiri kupiga kura.
Image caption Raia wa Zambia kwenye foleni wakisubiri kupiga kura.

Kiongozi wa upinzani nchini Zambia, Hakainde Hichilema, ameituhumu tume ya uchaguzi nchini humo kwamba imeshirikiana na chama tawala Patriotic Front, kufanya udanganyifu katika uchaguzi uliofanyika alhamisi iliyopita.

Chama cha Hakainde Hichilema, kimejiondoa kwenye mchakato wa kuhakiki kura, kutokana na madai ya udanganyifu.

Hakainde Hichilema ambaye anawania kiti cha urais kwa mara ya tano anadai kwamba kumekuwa na udanganyifu katika uchaguzi huo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Hakainde Hichilema, mwaniaji wa urais wa upinzani nchini Zambia

Chama chake kinataka kura za mji mkuu wa Lusaka zihesabiwe tena, akisema kulikuwa na dosari chungu nzima.

Mwaniaji wa chama tawala Edgar Lungu, amesalia kileleni, baada ya zaidi ya nusu ya kura zote kuhesabiwa.

Huenda kukatokea uchaguzi wa duru ya pili.

Marekebisho ya katiba ya hivi karibuni, yanahitaji mshindi apate zaidi ya asilmia 50 ya kura zote.

Wakati huo huo Rais Edgar Lungu amewataka raia wote wa Zambia kuwa watulivu na waheshimu mapenzi ya watu wengine.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Zambia, Edgar Lungu