Dalian Atkinson apigwa risasi na polisi ,Midlands

Uingereza

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Dalian Atkinson

mchezaji wa zamani wa ligi kuu ya Uingereza , Dalian Atkinson,amefariki dunia baada ya polisi kumfyatulia risasi kwakutumia bunduki ya kisasa yenye kasi zaidi.Polisi katika mji wa Midlands wamesema kwamba saa za alfajiri mwanzoni mwa wiki hii, wao waliitikia kile walichokiita 'wasiwasi kwa usalama wa mtu binafsi.

Wameendelea kuariku kuwa bunduki aina ya Taser ilitumiwa,na mwanamume mwenye umri wa miaka arobaini na nane, na kumtambua kama Atkinson, ambaye alifariki dunia wakatia akipatiwa matibabu.

Dalian Atkinson,amewahi kucheza katika vilabu kadhaa vikubwa vya mpira wa miguu kati ya miaka ya 1980 hadi miaka ya tisini, ikiwemo timu ya Aston Villa na Manchester City.