Rudisha ni mwamba wa mbio za mita 800

David Rudisha ahifadhi taji lake la OLimpiki
Image caption David Rudisha ahifadhi taji lake la OLimpiki

Mwanariadha raia wa Kenya amedhihirisha umwamba wake baada ya kushinda mbio za mita 800 huko Rio De Jeneiro nchini Brazil usiku wa kuamkia leo.

Mwanariadha huyo mwenye miaka 27 ameonyesha uzoefu wake katika mbio ambapo baada ya kuwa nyuma alianza kuwapita wenzake katika mzunguko wa mwisho na hata Mkenya mwenzake Alfred Kipketer na kukamilisha mbio hizo kwa dakika moja na sekunde 42.15

Naye Mualgeria Taoufik Makhloufi alishika nafasi ya pili na kujinyakulia medali ya fedha kwa kukimbia kwa dakika moja sekunde 42.61.

Mada zinazohusiana