Afisa wa Olimpiki akamatwa kwa wizi wa Tiketi

Patrick Hickey awekwa chini ya ulinzi
Image caption Patrick Hickey awekwa chini ya ulinzi

Mjumbe wa ngazi ya juu wa Kamati ya Olimpiki Patrick Hickey amewekwa chini ya ulinzi kwa kuhusishwa na ufisadi wa tiketi za Olimpiki.

Afisa huyo amejiuzulu kwa muda ili kupisha uchunguzi baada ya kuwekwa chini ya ulinzi kwa kuuza tiketi kinyume cha sheria.

Kumekuwa na uhudhuriaji mdogo katika michezo ya olimpic huko Rio ni kutokana na tiketi kuuzwa na baadhi ya maafsa kwa bei ya juu sana kimagendo.

Kukamatwa kwa Patrick Hickey, mmoja wa viongozi wa juu wa michezo ya Olympic ya ulaya, bado ni hoja kubwa kwa makao makuu ya polisi ya Brazil, kufuatia kukwamatwa kwa viongozi hao kumehusishwa kampuni ya kimataifa ya usimamizi wa michezo, THG.

Zaidi ya tiketi elfu moja za michezo ya olimpic zimesitishwa, ikiwemo tiketi za ufunguzi na zile za mbio za riadha, na wachunguzi wanasema madai ya udanganyifu yangeweza kutengeneza zaidi euro milioni mbili.

Kampuni hiyo ya kusimamia michezo ya kimataifa imekanusha shutma hizo huku jaji wa Brazil wiki hii akitoa agizo la kukamatwa washukiwa zaidi waliohusika na kesi hiyo.