Waogeleaji wawili wa Marekani wazuiwa kuondoka Brazil

Gunnar Bentz kushoto na Jack Conger walihojiwa na polisi Rio
Image caption Gunnar Bentz kushoto na Jack Conger walihojiwa na polisi Rio

Kamati ya Olimpiki nchini Marekani imethibitisha kwamba waogeleaji wawili wa taifa hilo wamezuiwa kuondoka nchini Brazil.

Hii ni baada ya polisi kutilia shaka habari walizotoa kuhusu kushambuliwa na kuporwa mali mjini Rio de Janeiro.

Polisi waliwatoa Gunnar Bentz na Jack Conger kutoka kwa ndege iliyokuwa ikielekea Marekani na kuwahoji.

Waogeleaji hao wawili, pamoja na wanamichezo wawili wa kikosi cha Marekani, wanasema waliporwa na watu wenye bunduki wakiwa kwenye teksi mjini Rio siku ya Jumapili.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bentz hakuwemo katika kikosi cha kuogelea 4x200m kupokezana mtindo wa freestyle fainali lakini bado alipokea medali ya dhahabu

Wanamichezo wenzao, Ryan Lochte na James Feigen, pia walizuiwa na jaji kuondoka Brazil.

Lochte tayari ameondoka nchini humo lakini taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema Feigen amezuiwa kuabiri ndege iliyokuwa inaelekea Marekani.