Mkenya ajiondoa katika mbio za mita 1500 Rio de Janeiro

Elija Manangoi kushoto na bingwa wa mbio za mita 1500 kulia
Image caption Elija Manangoi kushoto na bingwa wa mbio za mita 1500 kulia

Bingwa wa medali ya fedha katika mbio za mita 1500 Elijah Manangoi hatoshiriki katika mbio za siku ya Ijumaa mjini Rio baada ya kupata jeraha ,kulingana na mtandao wa Citizen Digital.

Manangoi ambaye alimaliza wa pili katika mbio za kufuzu za kundi la pili ili kuweza kufuzu katika fainali alipata jeraha na sasa ameshindwa kupona kwa wakati unaofaa ili kushiriki katika fainali hizo.

Katika taarifa iliojaa hisia katika mtandao wake wa facebook,Manangoi amethibitisha hatua hiyo,na kuwaombea ushindi wenzake waliosalia katika mbio hiyo Abel Kiprop na Richard Kwemoi.

Mada zinazohusiana