Waogeleaji wa Marekani washikiliwa Rio kwa mahojiano na polisi

Gunnar Bentz kushoto na Jack Conger walihojiwa na polisi Rio
Image caption Gunnar Bentz kushoto na Jack Conger walihojiwa na polisi Rio

Kamati ya Olimpiki nchini Marekani imethibitisha kuwa wanamichezo wake wawili wamezuiliwa kuondoka nchini Brazil baada ya polisi kusema kuwa kumeonekana kuwa na maelezo yasiofanana katika madai yao ya kuporwa mali mjini Rio.

Waogeleaji Jack Conger na Gunnar Bentz waliondolewa katika ndege zao siku ya Jumatano usiku kwa mahojiano na polisi.

Walikuwa miongoni mwa waogeleaji wanne kutoka bara la Amerika wanaosemekana kuporwa kwa kutishiwa na pastola siku ya Jumapili.

Image caption Waliondolewa katika ndege zao siku ya Jumatano usiku kwa mahojiano na polisi

Mahakama imeamuru wanamichezo hao wote wanne kusalia nchini Brazil kwa mahojiano zaidi.