Uber teksi kuzindua magari yanayojiendesha

Teksi za Uber Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Teksi za Uber

Kampuni ya teksi ya Uber kwa mara ya kwanza itazindua magari ya kujiendesha katika kipindi cha wiki mbili.Uber imesema kuwa uzinduzi huo utafanyika mjini Pittsburgh ,Pennysylvania.

Imeongezea kuwa inashirikiana na kampuni ya Volvo .

Kwanza magari hayo yatasimamiwa na dereva,ambaye atachukua udhibiti iwapo itahitajika,na muangalizi kulingana na Bloomberg.

Uber ina mpango wa kuwafuta kazi madereva wake milioni moja.

Msemaji wa kampuni hiyo ameiambia BBC kwamba kuanzia mwisho wa mwezi huu ,Uber itawaruhusu wateja wake mjini Pittsburgh kuyaita magari hayo yanayojiendesha ikiwa ni teknolojia ya hali ya juu ambayo haijaafikiwa duniani.

Mjini Pittsburgh ,wateja wataomba uchukuzi wa magari hayo kwa njia ya kawaida kupitia programu ya Uber,na itayashirikisha magari yanayojiendesha.

Uchukuzi utakuwa wa bure kwa sasa,badala ya kiwango cha kawaida cha dola 1.30 kwa kila maili moja.Kulikuwa na ripoti za kukanganya kuhusu magari ambayo yangeshiriki katika jaribio hilo.

Mada zinazohusiana